Aliyekuwa mgombea mwenza wa muungano wa Azimio ambaye pia ni kiongozi wa chama cha PLP Martha Karua anashikilia kuwa marehemu aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alifeli
pakubwa katika uchaguzi mkuu wa 2022.
Katika mahojiano kwenye Citizen TV mnamo Februari
26,2025 Karua alisema kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC marehemu Wafula
Chebukati alifeli pakubwa kulinda na kusimamia uchaguzi kwa njia ya haki na ya wazi.
Alifafanua akisema kuwa tukio la Marehemu Chebukati
kuwachukua makamishina wawili kamishina Abdi Guliye na Boya Molu dhidi ya
wenzake wanne wakiongozwa na Naibu mwenyekiti Juliana Cherera,Francis Wanderi,Irene
Masit na Justus Nyang’aya lilionyesha ukiukaji wa uwazi katika mchakato mzima.
Vilevile Bi Karua alieleza kuwa Mahakama pia ilichangia pakubwa
kuvuruga uchaguzi huo akisema kuwa maamuzi yake hayakuzingatia uzito wa walalamishi
ikizingatiwa kuwa idadi ya makamishina wanne dhidi ya wawili ilikuwa ni
idhibati tosha kuwa kulikuwa na dosari katika uchaguzi huo.
Uchaguzi wa mwaka wa 2022 ulifanyika Agosti 9,ambapo wawaniaji
wa kiti cha urais walikuwa ni wanne William Ruto wa UDA,Raila Odinga wa Azimio
la Umoja,George Wajakoya wa Roots Party na Wahiga Mwaure wa Agano Party.
Baada ya uchaguzi huo
William Ruto alitangazwa mshindi kwa kuzoa kura milioni saba,laki mia moja sabini
na sita mia moja arubaine na moja(7,176,141)
ambapo ilikuwa ni asilimia 50.5%, naye Bwana Odinga alipata jumla ya kura milioni
sita,laki mia tisa arubaine na mbili,mia tisa na thelathini(6,942,930) ambapo
ilikuwa ni asilimia 48.8% kulingana na mujibu wa IEBC.
Tangu uchaguzi huo kufanyika matukio mengi yametokea huku
vyama na viongozi kutoka upande wa serikali na upinzani vikishirikiana na wengine
kujiondoa kutoka kwa mirengo waliokuwa wakiegemea.
Karua alitangaza kujiondoa katika muungano wa azimio huku
aliyekuwa Waziri mkuu bwana Odinga akijenga ukuruba na serikali tawala ya Kenya
Kwanza na kuunda serikali jumuishi(BROAD
BASED GOVERNMENT).
Hata hivyo kulingana na kauli za bi Karua alionyesha ari ya
kujitosa kwenye debe ifakapo mwaka wa 2027 huku akiendeleza juhudi na jitihada
za kujiimarisha na kujenga urafiki na viongozi wengine wanaonekana kuikosoa
serikali ya Rais Ruto.
Bi Karua ,Bwana Stephen Kalonzo Musyoka ,Bwana Rigathi
Gachagua na Eugine Wamalwa kwa muda wa siku za hivi karibuni wameonekana kujenga
urafiki wa kisiasa na kukuwa na azma moja ya kuunda serikali ifikapo 2027.
Jambo ambalo Bi Karua alisema ni kuwa wanafanya juu chini
kupata ushawishi wa kutosha na kupata uungwaji mkono kutoka kwa kizazi cha Gen
Z ambacho kitakuwa na nguvu katika uchaguzi ujao wa 2027.